Ndi Umunyarwanda: Msingi wa Falisafa ya Umoja kwa Wanyarwanda
Go Back
Zaidi ya Miaka 27 imepita sasa tangu yafanyike Mauaji ya Halaiki ya Kimbari yaliyolenga jamii ya Watutsi nchini Rwanda.
Ni mauaji yaliyogharimu uhai wa Wanyarwanda zaidi ya Milioni Moja wasio na hatia na kuiacha jamii ya Wanyarwanda katika hali tete bila matumaini kabisa ya mustakabali wa taifa lao.
Mwaka huu (2021) imetimia miaka 25 tangu jumuiya ya Unity Club - Intwararumuri ianzishwe.
Hii ni jumuiya inayowakutanisha kwa pamoja Mawaziri waliopo madarakani na Mawaziri wastaafu pamoja na wenzi wao (wake/waume). Kwa Pamoja viongozi hawa huunganisha fikira na mawazo yao ya busara kukabiliana na changamoto zinazolikabili taifa ili waweze kutoa suruhisho la kudumu na lenye manufaa kwa taifa.
Unity Club ilianzishwa mwaka 1996, na Mheshimiwa Jeannette Kagame, mke wa Mheshimiwa Paul Kagame, Raisi wa sasa wa Jamhuri ya Rwanda. Akiwa na lengo la kujenga umoja wa Wanyarwanda kupitia viongozi wa juu ambao wamekuwa msitari wa mbele kutoa nuru na mwangaza (touch bearers) katika kuhamasisha jamii nzima (wazee na vijana) kuwa na umoja na uzalendo wa kweli, ili kulijenga taifa moja lenye nguvu, upendo na mshikamano.
Kupitia Jumuiya hii ya Unity Club, viongozi waliopo madarakani na wastaafu kutoka matabaka mbalimbali ya Wanyarwanda, kwa pamoja wamekuwa mfano bora katika kusimamia na kuenzi maadili mema kwa jamii ambalo ndilo lengo kuu la Unity Club, pamoja na kuchangia katika kujenga Umoja na Maridhiano miongoni mwa Wanyarwanda ili washirikiane katika kujenga jamii imara kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa Jeannette alijua wazi kuwa Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu na taifa la Rwanda lilikuwa na udhaifu mkubwa tangu awali katika suala hilo la kuwaunganisha wananchi jambo ambalo kulirekebisha ilihitajika ubunifu wa hali ya juu na mkakati wa kipekee katika mchakato mzima wa Serikali kuliunganisha taifa la Rwanda.
Kupitia mipango mbalimbali iliyoanzishwa na jumuiya hii ya Unity Club, wajumbe walitumia njia mbalimbali kujenga na kurudisha utu na upatanishi miongoni mwa jamii ya Wanyarwanda ikiwa ni pamoja na kupewa nasaha na mawaidha juu ya umuhimu wa umoja na mshikamano wa kitaifa ili kurekebisha makosa yaliyotokana na uwepo wa Sera za Kibaguzi zilizochangia kuwatenganisha Wanyarwanda katika matabaka yaliyochochea uhasama miongoni mwao.
Mheshimiwa Jeanneatte Kagame aliona ni vyema agenda hii ikaanzia kwa viongozi wa juu kama Mawaziri na familia zao ili kujenga umoja na uaminifu kati yao ili iwe rahisi kufikisha ujumbe huo kwa jamii kwa ujumla.
Ndi Umunyarwanda (Mimi Ni Mnyarwanda) ni programu (Mpango) mmojawapo kati ya mingi iliyobuniwa na kupewa kipaumbele chini ya jumuiya ya Unity Club ili kurejesha umoja na uaminifu katika jamii ya Wanyarwanda baada ya Mauaji ya Halaiki ya Kimbari ya mwaka 1994.
Katika Makala hii mpango huu wa Ndi Umunyarwanda utagusiwa na kujadiliwa kwa kina ili kuweka bayana maana na misingi yake.
Tafsiri rahisi ya neno Ndi umunyarwanda ni Mimi ni Mnyarwanda. Kwa mtazamo wa harakaharaka unaweza kujiuliza endapo Wanyarwanda kweli wanahitaji kukumbushwa uraia wao. Lakini kwa kuiangalia historia ya nchi ya Rwanda, tangu enzi za ukoloni na hata baada ya taifa kupata uhuru wa bendera, sera za kiutawala zilighubikwa zaidi na ubaguzi na viongozi walijikita zaidi katika kuwafundisha wananchi tofauti zao badala ya umoja wao. Hii ilikuwa kabla ya ukombozi wa Rwanda uliofanywa na wanajeshi wa RPA wa kulitoa taifa mikononi mwa uongozi dhalimu mnamo mwaka 1994.
Awali watu walitambuliwa kwa Ukabila zaidi (Mhutu, Mtutsi na Mtwa) na mbaya zaidi watu walipewa fursa ya elimu ama ajira kwa misingi ya ukabila na ubaguzi wa kikanda ambao ulishika hatamu.
Ilifikia mahali hata kitambulisho cha taifa (National Identity Card) kilikuwa na taarifa za kibaguzi za kikabila, na kikanda kama ilivyoainishwa hapo juu.
Ni dhahiri kabisa kwamba ubaguzi ulikuwa umekithiri kwa kiwango cha kutisha, ambapo harakati za viongozi kuitenganisha jamii zilipelekea kwa kiasi kikubwa kutokuaminiana, watu kutopata haki zao za msingi kwa sababu tu ya upande huu na sio ule.
Lilikuwa ni jambo la kawaida na viongozi waliona fahari kuwapendelea tu wale waliowataka wao pengine kwa kuwa wanatoka nao sehemu moja au kabila lao ni moja. Hii ilipalilia uhasama na chuki miongoni mwa Wanyarwanda
Baada ya ukombozi wa taifa uliofanywa na Jeshi la RPA likiongozwa na Jemedari Mkuu Paul Kagame, kurejesha utaifa badala ya ukabila, ilikuwa ni kazi kubwa na ilihitaji mipango na mikakati isiyo ya kawaida kuanza kuijenga Rwanda yenye umoja, upendo na mshikamano.
Zilihitajika mbinu madhubuti kukabiliana na majeraha ya aina mbalimbali iwe ya kimwili ama ya kisaikolojia. Ikumbukwe kwamba baadhi waliopoteza familia, ndugu jamaa na marafiki katika mauaji ya halaiki ya Kimbari dhidi ya Watutsi na wengine wakiuguzia majeraha makubwa yaliyopelekea ulemavu wa kimwili na hata kiakili,wajane na yatima wengi.
Wapo waliohusika katika mauaji ya Kimbari, au ndugu zao walihusika na walikuwa wanakabiliwa na mashitaka na adhabu kutokana na udhalimu huo. Wengine walikuwa wamezagaa huku na kule wakitafuta hifadhi ya ukimbizi. Wote walikuwa ni raia wa nchi ambayo haina hata taasisi moja inayofanya kazi na miundombinu yote ilikuwa imeharibiwa vibaya.
Kwa hiyo, kupitia Ndi Umunyarwanda ilikuwa ni fursa mpya inayowakumbusha na kuhamasisha Wanyarwanda kuwa na umoja na kujiona kama taifa moja lenye mwelekeo na lengo moja la kujenga nchi yao upya.
Uhamasishaji ulifanywa kupitia makongamano, warsha na vikao mbalimbali , na vyombo vya habari kama magazeti, majarida, radio na runinga.
Vijana, watoto na watu wazima wote walihusishwa ili kila mwananchi aweze kuwa na haki sawa na uwajibikaji katika kujenga taifa lake.
Kama ilivyoelezwa hapo awali, Unity Club - Intwararumuri kwa ushikiano na Tume ya Taifa ya Umoja na Maridhiani (National Unity and Reconciliation Commission) walianzisha Ndi Umunyarwanda programu mwaka 2013. Wajumbe wa UC walikuwa mstari wa mbele katika shughuli zote za uhamasishaji ndani na nje ya nchi hasa kupitia kwa Mabalozi kusudi hata Wanyarwanda walioko nje wasipitwe na fursa hii ya kuelewa ukweli na kuwa pamoja na wenzao katika kutafuta suluhu ya matatizo yanayoikabili nchi yao kama mchango wao wa kulijenga upya taifa la Rwanda.
Mafanikiyo ya Ndi Umunyarwanda.
Ilikuwa ni safari ndefu lakini yenye matumaini makubwa. Katika hiyo safari ambayo ni dhahiri kuwa bado inaendeleza mpango wa Ndi Umunyarwanda ambapo Programu ilifanikisha mambo mengi hasa kujenga na kukuza umoja wa Wanyarwanda na kurudisha hali ya kuaminiana na muhimu zaidi, kutoa mwongozo wa maadili mema kwa vijana ambao ni taifa la leo na kesho na ni nguzo muhimu kwa ustawi wa taifa lolote.
Katika utafiti uliofanywa mwaka 2020 kuangalia mchango wa Ndi Umunyarwanda katika kuleta umoja na maridhiano, matokeo yanatia moyo, asilimia 98 ya waliohusika wanakubaliana kwamba kuna mchango mukubwa wa Ndi Umunyarwanda katika kujenga na kuimarisha umoja na uaminifu miongoni mwa Wanyarwanda. Na asilimia 98 wanakubali kuwa Ndi Umunyarwanda imechangia kwa kiasi kikubwa kuwa na maadili mema miongoni mwa jamii.
Hivi sasa dhana ya ukabila na sera za ubaguzi zimepigwa marufuku. Kitambulisho cha taifa na cha kusafiria (passport) havina chembechembe za kibaguzi za kabila wala dini ya mmiliki wa vitambulisho hivyo.
Kupitia mpango huu wa Ndi Umunyarwanda, kumekuwa na michakato mbalimbali ya kuwakutanisha kwa mazungumzo ili kuombana radhi na kuridhiana kufuatia mauaji ya Kimbari yaliyowalenga Watutsi. Mchakato huo umepelekea watu hao kuishi pamoja kwa upendo na kusaidiana.
Wale ambao vidonda vyao bado ni vibichi au wanaugulia majeraha ya kihistoria kutokana na maovu ya sera chonganishi zilizowazilizowatenganisha Wanyarwanda wanaendelea kuuguza vidonda au makovu na wana matumaini ya kupona na kuwa na taifa moja lenye umoja na mshikamano katika kizazi hiki na vizazi vijavyo.
Wahenga walisema “Usione vyaelea vimeundwa”, Rwanda na Wanyarwanda baada ya janga la mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi mnamo mwaka 1994, ilikuwa ni jamii iliyosamabaratika. Miaka 27 baadae, leo Wanyarwanda wana matumaini ya maisha na wanauona mustakabali wao na wa taifa lao.
Hii inatokana na ukweli kuwa hivi sasa kupitia sera thabiti na mipango maridhawa kama huu wa Ndi Umunyarwanda na mipango mingine iliyopewa vipaumbele na serikali na wadau mbalimbali ikiwemo jumuiya ya Unity Club, wananchi sasa wanaishi kwa Amani na kuaminiana lakini yote haya hayajatokea kwa miujiza, bali ni mazao ya juhudi chanya na mikakati ya kipekee ya kuitoa nchi kwenye lindi la umasikini na sera za kikabila na ubaguzi wa kikanda, ikawa nchi ambayo kila Mnyarwanda ana haki sawa na uwajibikaji katika kujenga Rwanda mpya.
Unity club - Intwararumuri chini ya uongozi wa Mheshimiwa Jeannette Kagame ikishirikiana na taasisi nyingine za kitaifa imechangia kwa kiasi kikubwa katika kujenga umoja na maridhiano miongoni mwa Wanyarwanda.
Mimi ni Mnyarwanda!
Waandishi:
Coletha Uwineza RUHAMYA – Mjumbe wa Unity Club &
Hon. Oda GASINZIGWA – mjumbe wa Unity club na mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Latest updates
IMVO N’IMVANO Y’UBUNYAMURYANGO BUDACYURA IGIHE MURI UNITY CLUB
NEWSLETTER "INTWARARUMURI": JANUARY-JUNE, 2024
Ikinyamakuru INTWARARUMURI: Mutarama-Nyakanga, 2024
Newsletter Intwararumuri: July-December 2023
Ikinyamakuru Intwararumuri: Nyakanga-Ukuboza 2023
The closing ceremony of “Ndi Umunyarwanda” competition at the national level took place on February 4, 2022 at Lemigo Hotel Kigali
In December 2021, Unity Club members visited Intwaza and celebrated with them Christmas and a festive new year 2022
On December 6, 2022, Unity Club Joined by its Partners in Introducing the Second Phase of the Integrated Community Development Project in the Huye district
First Lady Jeannette Kagame, the Chairperson of Unity Club Called for Clear Transgenerational Ideology as Unity Club Marked 25 years
H.E. President Paul Kagame and First Lady Jeannette Kagame joined Unity Club’s 25th Anniversary Celebration
First Lady Jeannette Kagame, the Chairperson of Unity Club Joined Fellow Members, for the Annual General Assembly and Annual retreat
Ndi Umunyarwanda: Msingi wa Falisafa ya Umoja kwa Wanyarwanda
What’s in the name?
The impact of a shared cup of tea, bus trips on Unity Club’s remarkable beginnings of a journey to unity & reconciliation
Intwaza mu Mpinganzima zatwaje gitwari
1996–2021: Imyaka 25 irashize u Rwanda ruganura urumuri rw’ubumwe
Ndi Umunyarwanda, inkingi y’uburere buboneye mu muryango
Uruhare rw’Abarinzi b’Igihango mu kubaka Ubunyarwanda
Izingiro ry’uburezi bushingiye kuri Ndi Umunyarwanda
Uruhare rw’urubyiruko mu gushimangira Ubunyarwanda
Unity Club Intwararumuri is set to celebrate its 25th anniversary this year
Unity Club Intwararumuri has prepared competitions of Ndi Umunyarwanda for Higher Learning Institutions in order to encourage the youth to carry out research
Unity Club Intwararumuri reserves the month of June for the activities of strengthening Intwaza as one of the activities done under the 27th Commemoration of the Genocide against the Tutsi
On 18-19 May 2021, Unity Club Intwararumuri offered trainings to the guardians of covenant (Abarinzi b’Igihango) at national level
Ndi Umunyarwanda Platform on Radio Rwanda/ May 16, 2021: Ndi Umunyarwanda in public service
#Kwibuka27: Her Excellency First Lady Jeannette KAGAME, the Chairperson of Unity Club Intwararumuri asked the elders to teach the real history of Rwanda to the youth
#Kwibuka27: During the 27th commemoration period of the Genocide against Tutsi, Unity Club Intwararumuri prepared virtual talks to its members
#Kwibuka27: Ndi Umunyarwanda Platform on Radio Rwanda/ April 11, 2021: Gripping the covenant of Rwandan sprit
Ndi Umunyarwanda Platform on Radio Rwanda/ March 21, 2021: The woman’s role in strengthening Rwandan sprit
06 November 2020, Unity Club Intwararumuri annual retreat held at parliament
The contribution of Unity Club Intwararumuri in constructing total unity among Rwandans
31 October 2020, the 13th annual forum of Unity Club Intwararumuri takes place
October 2020: The month dedicated to promotion of unity and reconciliation: Unity Club played a vital role in different conversations teaching unity and reconciliation
September 27, 2020: Conversation on Ndi Umunyarwanda and patriotism
Ndi Umunyarwanda Platform on radio Rwanda/ August 16, 2020: Conversation on “Ndi Umunyarwanda in strengthening our education system”
The meaning and background of Intwararumuri
Rwandans are committed to strengthening and protecting Rwandan identity
Unity Club Inaugurates Homes For Elderly Genocide Widows
Huye : Mme Jeannette Kagame Yatashye "Impinganzima Hostel" Yagenewe Intwaza 100
Kirehe: Hashinzwe Ihuriro ryunganira Komisiyo y’Ubumwe n’Ubwiyunge na Unity Club
Akarere ka Rubavu kari ku mwanya wa 2 mu gihugu mu kugaragamo ingengabitekerezo ya Jenoside
Unity Club joins reconciliation drive
Abanyarwanda bakeneye ubumwe n’ubwiyunge budacagase- Min Nsengimana
Unity Club tips Nyagatare officials on reconciliation
Ihuriro ry’Ubumwe n’Ubwiyunge ku rwego rw’Akarere
Nsanzabaganwa honoured by SU-SA for her role in developing academically Sound Economic Policies
Perezida Kagame Na Madamu Jeannette Kagame Bifurije Abana Noheri Nziza Ya 2016
Perezida Kagame Ntashidikanya Ku Iterambere Ry’u Rwanda Mu Myaka 22 Ishize
The 17 Protectors Of Friendship Pact (Abarinzi B’Igihango)
First Lady Jeannette Kagame Honoured By Unity Club
The President Of Unity Club Awarded Seventeen People For Their High Humanity During The Genocide
First Lady : Integrity Among Leaders Key To National Unity
Aho Ubumwe butari ingaruka ziba mbi – Perezida Kagame
Kuzaraga Abana Igihugu Kizira Ikibi Ni Inshingano Zacu – Jeannette Kagame
Unity Club Intwarumuri Nyuma Y’imyaka 20 Ibayeho
Unity Club Lays The Foundation For A Home For 100 Elderly Survivors Living Alone
Abana B’imfubyi Barerwaga Na Unity Club Batangiye Kubaka Ingo Zabo
Madamu Jeannette Kagame Yashyikirije Amacumbi Incike Za Jenoside
Unity Club To Build Hostel For 100 Genocide Widows
Global Women Forum Discusses Gender Parity, Financial Freedom
Jeannette Kagame Yasabye Abagore Kutirara Kubera Politiki Yabahaye Byose
Rwanda’s Journey Of Women Empowerment
Rwanda’s March Towards Gender Parity By 2030
U Rwanda N’abafatanyabikorwa Mpuzamahanga Mw’ishoramari Ry’abagore
Buri Wese Akwiye Kubungabunga Iterambere N’ubusugire Bw’igihugu - Jeannette Kagame
Make Unity Our Legacy For Next Generations : First Lady
Unity Club Yishimiye Uko Igikorwa Cyo Gutoranya Abarinzi B’Igihango Kirimo Gukorwa
Urubyiruko rwo mu karere ka Nyamagabe rwakanguriwe gukumira no kurwanya ihakana n’ipfobya rya Jenoside yakorewe Abatutsi muri Mata 1994
Nyuma Yo Kubakirwa Ishuri Ry’incuke Banahawe N’ikibuga Cy’imyidagaduro
IMPINGA NZIMA, Kimwe Mu Bisubizo Ku Ncike Za Jenoside Yakorewe Abatutsi
Our Differences Should Be Our Strength, Kagame Tells Leaders
Perezida Kagame Ntabwo Yumva Ukuntu Nyuma Y’imyaka 20 Abantu Badakura Isomo Mu Mateka Yahise N’ibyiza Bimaze Kugerwaho
“Ndi Umunyarwanda” Ni Urugendo Rugikomeza - Jeannette Kagame
Inama Ngarukamwaka Ya 7 Ya Unity Club Irabera Kuri Serena Hotel I Kigali
Nyamagabe : First Lady Tells Cyanika Residents To Strive To Make Self-Reliance A Reality
Nyamagabe: Madamu Jeannette Kagame Yatashye Ibikorwa Bitandukanye Asaba Abaturage Kubibungabunga
"Ndi Umunyarwanda" Yaje Kuzuza Gahunda Zisanzwe Z’ubumwe N’ubwiyunge
“Ndi Umunyarwanda” Yubaka Ubunyarwanda Kuruta Aho Umuntu Yavukiye
Nyamasheke : “Ndi Umunyarwanda” Yagejejwe Mu Mashuri Yisumbuye
"Ndi Umunyarwanda" Is About Healing The Genocide Wounds
First Lady Hands Over New 20 Houses To Orphans
Imfubyi Zo Ku Nyundo Zasangiye Noheri Na Madamu Jeannette Kagame Anazishyikiriza Amazu 20
Ndi Umunyarwanda: Dr Habumuremyi Regrets His Inaction During The Genocide
Karongi : «Ndi Umunyarwanda» Irimo Gutanga Umusaruro Mwiza
“Ndi Umunyarwanda” Ni Umwanya Wo Gutekereza Ku Isano Y’Abanyarwanda - Nsanzabaganwa
Minisitiri Murekezi Yasabye Imbabazi Ku Ibaruwa Yasabaga Ko Abatutsi Basubizwa Inyuma
Yasabye Imbabazi Abahutu Kuko Ngo Yajyaga Ababona Nk’abagome Bose
“Nta Macenga Ya Politiki Ari Muri Gahunda Ya ‘Ndi Umunyarwanda’”- Gov. Bosenibamwe
Kayonza : Abayobozi Barasabwa Guha Ijambo Abaturage Muri Gahunda Ya “Ndi Umunyarwanda” Kugira Ngo Babohoke
Nyamagabe: Abantu Barirekuye Basaba Imbabazi Mu Mwiherero Wa “Ndi Umunyarwanda”
Depite Bamporiki yanenze ibyo Abahutu bakomoka iwabo bakoreye bene wabo b’Abatutsi
Abarwanya “Ndi Umunyarwanda” Ni Abababazwa N’iterambere - Gov. Uwamariya
Ngoma : Abayobozi Ngo Babashije Gusobanurirwa Gahunda Ya “Ndi Umunyarwanda”
"Gusaba Imbabazi Si Agahato, Abatariyakira Urugendo Ruracyakomeza"
First Lady Wins Global Leader Award
Food For New Village Project Launched The Land Terracing Activities In Cyanika Sector
Food For New Village Project Started Water Supply Activities In Cyanika Sector
Upholding Inyumba’s Legacy
Unity Club Organizes Fifth Consultative Forum
Unity Club Intwararumuri mw’Ihuriro ngarukamwaka rya gatanu (5)
Rwandans Reconciled At Over 80%
Rwanda’s Strength Is Its Unity–Kagame
Unity Club Intwararumuri mu Ihuriro ngarukamwaka rya gatanu
Igisikare Na Polisi Mu Gikorwa Cyo Kubaka Amazu Y’abana B’imfubyi Zo Ku Nyundo
Unity Club Yahawe Amafaranga Miliyoni 15 Na BRALIRWA Agenewe Kubakira Impfubyi 20 Zo Mu Kigo Cya Nyundo
Food For New Village Built Two Classrooms At Cyanika Sector
First Lady Opens Cyanika Genocide Memorial
Fundraising For Nyundo Children In Rubavu
Unity Club Yateye Inkunga Urwibutso Rwa Jenoside Rwa Cyanika-Nyamagabe
Minisitiri W’Intebe Yatangije Gahunda Yo Kubakira Amazu 20 Abana B’imfubyi Zo Ku Nyundo
Unity Club Witnessed The Signing Of MoU Between WFP And Good Neighbors Rwanda
Unity Club izubakira abana 20 bafite imyaka 18 bo muri Orphelinat Noel
PM Joins Rubavu Orphans In Xmas Party
2011 Unity Club Award Ceremony
Ubutwari bwo kubaho Association Win 2011 Unity Award
Unity Club Gets Frw 5m From Bralirwa To Renovate Cyanika Memorial Site
More Than 150 Children, Mostly Orphans And Disabled, Celebrated The Christmas Party At Village Urugwiro
Children’s Christmas Party At Village Urugwiro
Word From The Chairperson Of Unity Club
Congratulation Message
Unity Club Honours Kagame
More Updates
News and Events
Go to News and EventsArticles
Go to ArticlesPublications
Go to publications